ZAINA FOUNDATION IMEZINDUA KAMPENI YA UHAMASISHAJI JUU YA KUPATIKANA MTANDAO MUDA WOTE KIPINDI CHA UCHAGUZI LEO – JUNE 24, 2020.

Taasisi ya Zaina foundation inayoshughulika na kuwainuwa wanawake katika maatumizi ya teknolojia pamoja na mtandao.  imezindua kampeni maalumu iitwayo #KeepItOnTz au #NaIwakeIntaneti ikiwa na  lengo la kuhamasisha upatikanaji wa mtandao kipindi vyote cha uchaguzi ili kuwawezesha watanzania  kupata taarifa zinazohusu uchaguzi na kampeni kwa wakati

Mkurugenzi mtendaji Zaina Foundation Anasema kuwa  kampeni hii inalenga kuhamasisha serikali na mamlaka na mamlaka zinazohusika na mawasiliano kuhakikisha upatikanaji wa mtandao katika kipindi chote cha uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu 2020 na kupunguzwa kwa gharama za matumizi ya mitandao ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hiyo hat kwa wanawake wenye kipato cha chini.

“Lakini pia makampuni ya simu kuweka gharama nafuu za vifurushi vya intanet ili kuwezesha hata wananchi wenye kipato cha chini kupata huduma  ili na wao wapate taarifa kipindi hiki cha uchaguzi” amesema   Njovu.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo  anasisitiza kuwa maeneo kadhaa  ya vijijini huwa yanakuwa na changamoto ya upatikanaji wa mtandao hivyo  anatoa wito kwa mamlaka kuhakikisha zinaboresha mifumo ya mitandao ili katika kipindi chote hicho watanzania waweze kupata taarifa bila matatizo yoyote. Na kueleza dhamira ya taasisi hiyo kuendelea kutoa elimu kwa watanzania kuhusu matumizi bora ya mtandao.

“Pia tunataka elimu kupitia mitandao ya kijamii na tunawaalika watanzania wote kutusaidia kutoa taarifa pale wanapata matatizo ya mitandao ili na sisi tuweze kuona namna ya kuwasaidia kufanikisha kero zao kwa mamlaka husika Amesema ” Zaituni Njovu.

Mitandao ya kijamii imekuwa ni nyenzo muhimu  ya kurahisisha upatikanaji wa taarifa Katika kipindi hiki tunapoelekea uchaguzi ni haki ya kila mtanzania kupata taarifa sahihi zinazohusu uchaguzi lakini pia wagombea wana nafasi kubwa ya kunadi sera zao kupitia mitandao ya kijamii.

#KeepItOnTz #NaIwakeIntaneti

Leave a Reply

Your email address will not be published.

X